🗓️ TAREHE KUU ZA UCHAGUZI MKUU

  • Jisajili ili upige kura tarehe 23 Oktoba.

  • Tuma omba la kura ya barua ya posta tarehe 31 Oktoba. Inapendekezwa kuwa uwasilishe ombi kabla ya tarehe 20 Oktoba.

  • Rudisha kura ya barua ya posta kabla ya saa 8 p.m. tarehe 7 Novemba. Inapendekezwa kuwa uirudishe kabla ya tarehe 1 Novemba.

TAARIFA KWA WAPIGA KURA WALIOKO PENNSYLVANIA:

🗳️ Kuna uchaguzi JUMANNE, NOVEMBA 7.

Je, hujawahi kujisajili hapo awali? Je, umehama tangu ulipopiga kura mara ya mwisho?

Ikiwa hujawahi kupiga kura hapo awali, hatua ya kwanza ni kujisajili. Ikiwa chochote kimebadilika tangu mara ya mwisho ulipopiga kura - umebadilisha anwani, umebadilisha jina au unataka kubadilisha chama chako - unapaswa kusasisha usajili wako. Ni muhimu kujisajili katika anwani yako ya sasa ili uweze kupiga kura sahihi, hasa ikiwa unapanga kupiga kura kwa barua ya posta.

Tarehe Kuu za Kupiga Kura kwa Barua ya Posta au Bila Kuhudhuria Kituo cha Kupiga Kura

Ikiwa unataka kujisajili ana kwa ana, au kwa karatasi, piga simu namba ni 1-877-VOTESPA ili upate usaidizi.



UNA HAKI!

Unaweza kujisajili na kupiga kura ikiwa:

  • Wewe ni raia wa Marekani

  • Una umri wa miaka 18 au zaidi ifikapo Siku ya Uchaguzi

  • Wewe ni mkaazi wa Pennsylvania

☎ Kila mtu anayestahiki ana haki ya kupiga kura. Ili kupata maelezo yaliyosasishwa kuhusu uchaguzi, kupata usaidizi kuhusu suala lolote linalohusiana na kupiga kura, au kuripoti tatizo katika Siku ya Uchaguzi, unaweza kupiga simu kwa mojawapo ya namba hizi za dharura zisizopendelea chama chochote:

  • Kiingereza: 866-OUR-VOTE (866-687-8683)

    Kamati ya Mawakili ya Haki za Kiraia Chini ya Sheria

  • Kihispania na Kiingereza: 888-VE-Y-VOTA (888-839-8682)

    Mfuko wa Elimu wa NALEO

  • (عربى Kiarabu na Kiingereza: 844-YALLA-US (844-925-5287)

    Taasisi ya Kiarabu ya Marekani (AAI)

  • Kimandarini, Kikantoni, Kikorea, Kivietinamu, Kitagalogi, Kiurdu, Kihindi, Kibengali na Kiingereza - 888-API-VOTE (888-274-8683)

    APIAVote & Asian Americans Advancing Justice (AAJC)

  • Simu ya video ya lugha ya ishara ya Marekani: 301-818-VOTE (8683)

    Chama cha Kitaifa cha Viziwi (NAD)

📞 Unaweza pia kupigia simu ofisi ya uchaguzi ya jimbo ili upate usaidizi, ikiwa ni pamoja na jinsi ya kupata ofisi ya uchaguzi ya jiji au kaunti yako: 1-877-VOTESPA


JUA HAKI ZAKO!

KUJISAJILI KUPIGA KURA

Nilijisajili kupiga kura hivi majuzi. Je, nitahakikisha vipi kuwa nimesajiliwa?

Inachukua siku chache ili ofisi ya uchaguzi ya kaunti ipitie fomu yako ya usajili na iandike jina lako kwenye orodha.

Mimi ni mpiga kura aliyesajiliwa, lakini nilihama hivi majuzi. Je, bado nimejisajili kupiga kura?

  • Ndiyo. Ila, ikiwa ungependa kupiga kura karibu na nyumba yako mpya, au ikiwa unataka kupiga kura kwa njia ya barua ya posta, utahitaji kusasisha usajili wako kwa kuandika anwani yako mpya. Unaweza kubadilisha anwani yako mtandaoni katika Idara ya Jimbo ya PA. Ikiwa unataka kujisajili ana kwa ana, au kwa karatasi, piga simu namba ni 1-877-VOTESPA ili upate usaidizi.

  • Unaweza pia kurudi kwenye kituo chako cha zamani cha kupigia kura na upige kura huko. Iwapo ulihama chini ya siku 30 kabla ya uchaguzi, ni lazima upige kura katika kituo chako cha zamani cha kupigia kura. Ikiwa ulihama kutoka nje ya jimbo, unahitaji kujisajili kupiga kura hapo Pennsylvania.

Je, ninaweza kujisajili na kupiga kura ikiwa nimeshtakiwa kwa kuhusika katika uhalifu?

  • Ndiyo, unaweza kupiga kura mradi haujafungwa kwa kosa la jinai kwa sasa. Unaweza kupiga kura ikiwa uko katika kipindi cha majaribio au kifungo cha nje, ukiwa chini ya kifungo cha nyumbani, au ikiwa unatumikia kifungo kwa ajili ya kosa dogo.

Nilizaliwa Puerto Rico. Je, ninaweza kupiga kura katika jimbo la Pennsylvania?

  • Ikiwa ulizaliwa Puerto Rico, wewe ni raia wa Marekani kiotomatiki na unaweza kujisajili kupiga kura katika jimbo la Pennsylvania (au jimbo unaloishi).

Kupiga kura au hata kujisajili kupiga kura wakati wewe si raia wa Marekani ni uhalifu na kunaweza kukuzuia kuwa raia.


📨 KUPIGA KURA KWA BARUA YA POSTA

Je, ninatuma vipi ombi la kura ya barua ya posta?

Unaweza kutuma ombi la kura ya barua ya posta kwa njia 3:

  1. Tuma ombi la kura ya barua au ya kutohudhuria kituo cha kupigia kura kwa www.vote.pa.gov.

  2. Pakua na ujaze ombi la karatasi kutoka kwa www.vote.pa.gov.

  3. Tuma ombi katika ofisi yako ya uchaguzi ya kaunti.

Je, nifanye nini ikiwa ombi langu la kura ya barua ya posta limekataliwa?

  • Ukipata notisi kwamba ombi lako lilikataliwa, piga simu kwa 866-OUR-VOTE ili usaidiwe bure na wakili. 

Nitapata kura yangu lini?

  • Kwa mujibu wa sheria, lazima kaunti ikutumie kura yako ya barua ya posta wiki mbili kabla ya uchaguzi. Iwapo haitafika, au ukiipoteza, au ukifanya makosa unapotia alama kwenye kura, pigia simu ofisi yako ya uchaguzi ya kaunti ili wakupe nyingine.

  • Unaweza kuangalia au kufuatilia kura yako kwenye www.vote.pa.gov/mailballotstatus.

Je, mtu mwingine anaweza kunipelekea kura yangu ya barua ya posta?

Je, ninaweza kubadilisha mawazo yangu kuhusu kupiga kura kwa barua ya posta baada ya kutuma ombi?

  • Ndiyo. Lete kura yako na bahasha ya kurejesha katika kituo chako cha kupigia kura Siku ya Uchaguzi. Wafanyikazi wa kura wataighairi, na unaweza kupiga kura ana kwa ana katika kituo cha kupigia kura. Ikiwa huna kura yako, itabidi upige kura ya muda.

Je, kura yangu itahesabiwa kweli nikipiga kura kwa barua ya posta?

  • Kupiga kura kwa barua ya posta ni salama. Kuna ukaguzi unaofanya ili kuhakikisha kuwa kura yako inahesabiwa. Ikiwa unashuku kuwa kura imepotea katika barua ya posta, au ukiipoteza nyumbani, unaweza kupigia simu ofisi yako ya uchaguzi ya kaunti na kuomba nyingine. Tafuta ofisi ya uchaguzi ya kaunti yako kwenye Google, au upige simu kwa 1-877-VOTESPA ili uunganishwe

Ili kura yako ihesabiwe lazima:

  • Uingize kura yako iliyotiwa alama kwenye bahasha ya siri, iliyoandikwa "Kura Rasmi ya Uchaguzi." Funga bahasha na usiandike chochote kwenye bahasha hiyo

  • Uingize bahasha ya siri iliyofungwa kwenye bahasha ya nje ya kurejesha yenye anwani ya kaunti

  • LAZIMA utie sahihi kwa kuandika jina lako na tarehe kwa mkono kwenye bahasha ya kurejesha.

  • Usipotia sahihi na kuandika tarehe kwenye bahasha kura yako HAITAHESABIWA.


👋 KUPIGA KURA ANA KWA ANA

Ninapaswa kupiga kura wapi?

  • Unaweza kupata kituo chako cha kupigia kura kwenye www.vote.pa.gov, kwa kupiga simu kwa 866-OUR-VOTE au kwa kupigia simu afisi yako ya uchaguzi ya kaunti.

Je, ninahitaji kitambulisho cha picha ili nipige kura ana kwa ana?

  • Hapana. Wapiga kura wanaopiga kura kwa mara ya kwanza katika kituo chao cha kupigia kura pekee ndio wanahitaji kuonyesha kitambulisho. Unaweza kutumia kitambulisho cha picha, ikiwa ni pamoja na kitambulisho cha mfanyakazi au mwanafunzi ikiwa unayo. Unaweza pia kutumia kitambulisho kisicho cha picha, kama vile bili ya huduma au taarifa ya benki iliyo na anwani yako. Hupaswi kuombwa kitambulisho chako ikiwa ulipiga kura hapo awali katika kituo hicho cha kupigia kura.

Je, wakiniambia kuwa jina langu halipo kwenye orodha ya wapiga kura?

  • Kwanza, mwombe afisa wa uchaguzi aangalie orodha tena au aangalie kitabu cha ziada cha kura (orodha ya mabadiliko ya hivi majuzi kwenye orodha za wapiga kura). Jitolee kutamka jina lako. Ikiwa unaamini kuwa uko katika kituo sahihi cha kupigia kura lakini jina lako haliko kwenye orodha ya wapiga kura, omba kura ya muda, wanatakiwa kukupa. Tafadhali ripoti mambo uliyopitia kwa 866-OUR-VOTE.

Je, kura ya muda ni nini?

  • Kura ya muda hutumika kurekodi kura yako wakati kuna swali kuhusu ustahiki wako au ikiwa uliomba kura ya barua ya posta. Itahesabiwa iwapo maafisa wa uchaguzi watabaini kuwa ulistahiki kupiga kura. 

Je, haki yangu ya kupiga kura inaweza kupingwa katika kituo cha kupigia kura?

  • Ndiyo, lakini kwa sababu fulani na watu fulani. Afisa wa uchaguzi, mwangalizi wa shughuli za kupiga kura, au mpiga kura mwingine anaweza tu kumpinga mpiga kura ikiwa anafikiri kuwa mpiga kura huyo haishi katika jimbo la uchaguzi au ni mtu anayejifanya mtu mwingine.


Kanusho

Mwongozo huu wa kupiga kura katika jimbo la Pennsylvania sio ushauri wa kisheria. Ikiwa una maswali kuhusu kustahiki au haki zako, tafadhali piga simu kwa 866-OUR-VOTE au wasiliana na wakili.

Kwa taarifa zaidi, tembelea www.vote.pa.gov.